.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 15 Agosti 2015

NAIBU WAZIRI WA MAJI, MH AMOS MAKALLA ATEMBELEA MRADI WA MAJI WILAYANI SENGEREMA

Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akimsikiliza mhandisi mshauri wa kampuni ya COWI ndg Michael Nyagabona.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla ( mwenye miwani ) kipokea maelezo toka kwa mkurugenzi wa mamlaka maji mwanza eng Antony Sanga.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akiongea na waandishi habari eneo la Igogo.

Naibu waziri wa maji Amos G. Makalla amefanya ziara ya kikazi wilaya ya Sengerema kwa kukagua ujenzi wa mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika na serikali ya Tanzania.

Mradi huu unagharimu shilingi bilioni 20 na utanufaisha watu wapatao 108,000 hadi kufikia mwaka 2025.
Naibu Waziri wa Maji ametembelea chanzo cha maji ziwa victoria kijiji cha Nyamazugo, ujenzi wa matanki maeneo ya Mwabaluhi na Igogo na kuwataka wakandarasi kampuni ya Kichina Ya CCECC ltd na mhandisi mshauri kampuni ya COWI kuongeza kasi ya ujenzi na kukamilisha ujenzi wa mradi ifikapo Februari 2016.
Aidha ameagiza mkandarasi kuanza ulazaji wa mabomba kutoka tanki la Nyamazugo kwenda tanki la Igogo ili kuharakisha upatikanaji wa maji.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano wakati mradi huu unatekelezwa kwani kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wao wananchi wa sengerema.
Amepongeza jitihada za mkuu wa wilaya ya sengerema na mamlaka ya Maji mkoa wa Mwanza kwa pamoja wamewezesha mradi kufikia hatua nzuri

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni