.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 19 Agosti 2015

NAIBU WAZIRI WA MAJI, MH AMOS MAKALLA AKAGUA MRADI MKUBWA WA MAJI BUNDA

Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akisaini kitabu ofisi za ccm wilaya ya Bunda.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla ( kulia ) akiwa na aliyekuwa mbunge wa Mwibara ndugu Kangi Lugola wakiwakiliza watalaam wa mradi.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akikagua ulazaji wa mabomba mji wa Bunda.
Mh Amos Makalla ( wa pili kutoka kushoto ) akikagua shehena ya mabomba yatakayitumika kwa usambazaji mji wa Bunda
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akipokelewa na mkuu wa wilaya ya Bunda ndugu Joshua Mirumbe.

Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla amekagua mradi mkubwa wa maji utakaohudumia wananchi wa mji wa Bunda na vijiji 13 vilivyopo karibu na chanzo na vitakavyopitiwa na bomba kuelekea mji wa Bunda.

Kwa mujibu wa injinia Gantala Gantala, Mkurugenzi wa mamlaka ya maji Musoma ambao ndiyo wasimamizi wa ujenzi wa mradi huo kwa niaba ya Wizara ya Maji, ameeleza kuwa mahitaji ya maji sasa kwa wananchi wa mji wa Bunda ni lita milioni 5 kwa siku, wakati uzalishaji wa sasa maji ni lita milioni moja na laki mbili tu. 

Kutokana na hali hiyo, amesema mradi huu umekusudia kuzalisha maji lita milioni 8 kwa siku na hivyo kumaliza kabisa tatizo la maji mji wa Bunda na vijiji 13.

Mradi wa maji Bunda unagharimu fedha shilingi bilioni 8 na umetekelezwa kwa awamu nne na utakamilika mwishoni mwa mwezi Septemba.

Aidha naibu Waziri wa Maji amemwagiza mhandisi wa maji wilaya ya Bunda kufanya usanifu wa vijiji vya Busimbwe, Bulamba na Mwiseni vilivyoko karibu na chanzo ili vipatiwe maji ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda aliyoitoa mwezi mei mwaka huu wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji iliyofanyika Bunda.

Amewataka wakandarasi wote wa mabomba kutoka katika chanzo na mkandarasi wa mabomba usambazaji mjini kukamilisha mradi mwezi septemba kama walivyohaidi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni