Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza rasmi kujiuzulu
wadhifa huo na kubakia kuwa mwanachama wa kawaida.
Akiongea na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es Salaam Prof. Lipumba amesema amechukua uamuzi huo
kutokana na kukiukwa kwa mambo kadhaa na Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha
CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akizungumza na Wandishi wa
habari katika moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Peacok hotel jijini
Dar leo kuhusiana na kung'atuka kwake rasmi Uenyekiti wa chama hicho
na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida,ambapo Mh Lipumba ameeleza
kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama hai na halali wa kawaida kwa sababu
kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha
CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida
kulia, Abdala Shabani pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa
wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na
waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam
leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha
CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha rasimu ya Katiba
pendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndio
iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)
katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya
Peacock jijini Dar es Salaam leo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni