.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 30 Agosti 2015

ROSE MUHANDO KUPAMBA TAMASHA LA AMANI DAR


MWIMBAJI wa muziki wa injili Rose Mhando amethibitisha rasmi kushiriki katika Tamasha kubwa la kihistoria la kuiombea Amani nchi kuelekea uchaguzi mkuu linarotarajia kufanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa kabla ya kwenda mikoani.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama, alisema Mhando tayari amethibitisha kuimba siku hiyo, ambako tayari ameshaanza maandalizi ikiwa pamoja na nyimbo mpya ambazo ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha amani.

Msama alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo la kihistoria yanaendelea vizuri ikiwa pamoja na waimbaji kujiandaa vizuri watakuwepo waimbaji kutoka nchi zaidi ya tano kuungana na watanzania katika tukio hilo ambalo litashirikisha matukio mbalimbali.

Aidha Msama alisema kuwa mbali ya kuliombea taifa amani kuelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.



Alisema kuwa waimbaji wengine wanaendelea kuthibitisha ambapo pia mbali ya kuimba mmojammoja wataimba wimbo wa pamoja ambao umeandaliwa, hivyo Msama aliwaomba watanzania kujitokeza katika tukio hilo muhimu la kitaifa.

Naye Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Beno John Chelele alisema tamasha hilo ni la muhimu hasa katika kipindi hiki cha uhaguzi ambao umekuwa wa tofauti na chaguzi zilizowahi kufanyika miaka ya nyuma.

“Kila Mtanzania ashiriki tuliombee taifa letu kokote litakakopita tamasha hili ni la muhimu hasa katika wakati huu wa uchaguzi ambao ni wa aina yake,” alisema Beno.

Tamasha hilo litanzia mkoa wa Dar es Salaam Oktoba 4, Morogoro Oktoba 7, Iringa 9,Mbeya Oktoba 11, Dodoma Oktoba 14, Shinyanga Oktoba 16 na kumaliziwa na Mwanza Oktoba 18.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni