.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 5 Agosti 2015

TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TANZANIA ( TASWA )

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA), inatarajiwa kukutana Ijumaa Agosti 7, 2015, Dar es Salaam
kujadili masuala mbalimbali yahusiyo michezo na waandishi wa habari za
michezo hapa nchini.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitajadili namna bora ambayo chama
kinaweza kushiriki kwa kuangalia jinsi ya kuwaunganisha wanamichezo kwa
namna mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwa maslahi ya michezo nchini.

Moja ya madhumuni ya TASWA wakati inaanzishwa ni kuwaunganisha waandishi wa habari za michezo nchini, kushirikiana katika kukuza na
kupromoti michezo na wanamichezo kwa njia ya kalamu na njia nyingine za
kupashana habari.

Kwa msingi huo tunaamini kikao kitatoa muongozo mzuri, ambao unaweza
ukasaidia wanamichezo hapa nchini kufahamu sera za michezo kwa wagombea
mbalimbali na hivyo kufanya uamuzi sahihi wakati ukifika.

Pia kikao kinatarajiwa kufanya uteuzi wa washiriki wa semina mbili
zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni, zikihusisha waandishi wa habari
za michezo wa kada ya kati na wale wazoefu.

Tunaamini tumetoka mbali na tunajua safari yetu ya kuchangia kukuza
michezo nchini bado ni ndefu na ina mabonde, mabwawa na utelezi. Sisi
hatujiulizi , Jee tutafika? Bali hujiambia juhudi zetu zitatufikisha
tunapotaka kufika.

B; PONGEZI AZAM


Tunatoa pongezi kwa timu ya soka ya Azam FC kwa kuibuka bingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’mwaka 2015.

Tunaungana na Watanzania wengine katika kufurahia ubingwa huu, baada ya
Jumapili Azam kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mchezo wa
fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hivyo tunawaomba wachezaji
watumie ubingwa wa Kagame kama changamoto ya kufanya vizuri katika
michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwakani.

Azam wasibweteke na kuona tayari wamemaliza kazi, bali waendelee na
jitihada za kutafuta mafanikio makubwa zaidi.

C: UTOAJI WA VITAMBULISHO

TASWA ilisitisha kutoa vitambulisho vipya kwa wanachama wake kwa muda
kwa sababu ilikuwa ikifanya utaratibu wa kubadili vile vya awali na kuwa
na vitambulisho vya kisasa zaidi, ambapo suala hilo lipo hatua za mwisho
kukamilika na hivi karibuni wanachama wote wapya watapatiwa vitambulisho
vyao.

                                                                                              Nawasilisha,
                                                                                            Amir Mhando,
                                                                                    Katibu Mkuu TASWA

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni