Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambi rambi kwa familia ya Muro, kufutia kifo cha Mzee Cornel Muro kilichotokea mwishoni mwa wiki jijini Dar s salaam na mazishi kufanyika Machame mkoani Kilimanjaro.
Katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya marehemu Muro, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo na kuomba mwenyezi Mungu awajilie nguzu wafiwa
Marehemu Cornel Muro ni baba mzazi wa Afisa Habari wa klabu ya Young Africans, Jerry Muro.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni