Aliyekuwa kiongozi wa Chad Hissene
Habre ameburuzwa kortini na walinzi weliofunika sura zao wakati wa
kuanza kwa kesi yake ya ya uhalifu wa kivita katika Jiji la Dakar
nchini Senegali.
Kiongozi huyo wa zamani wa Chad
aliingizwa mahakamani kwa kutumia nguvu baada ya kugoma kwenda, na
pia alikatiza usikilizaji wa kesi kwa kupiga kelele wakati akisomewa
mashtaka.
Habre anatuhumiwa kwa kuagiza mauaji
ya watu 40,000 wakati wa utawala wake katika miaka ya 1980, mashtaka
ambayo amekanusha.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni