Basi la Metro lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, limepinduka katika eneo la Manga, wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Katika ajali hiyo, watu 5 wamefariki dunia na wengine 39 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo, ambaye alishindwa kulimudu basi hilo wakati alipofika katika eneo lenye kona na hivyo kusababisha kupinduka.
Kamanda Mwombeji amesema baada ya ajali hiyo, dereva alikimbia na jeshi la polisi linaendelea kumsaka ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni