.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 20 Septemba 2015

DK. SHEIN AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM JIMBO LA MICHEWENI

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi wa Jimbo la Micheweni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba katika Mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu pamoja na kuwaombea kura Mgombea Urais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Mgombea Mwenza,pia wakiwemo wagombea Ubunge,Uwakilishi na Udiwani. Picha zote na Ikulu.
6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiwatambulisha wagombea Udiwani CCM Majimbo ya Uchaguzi Mkoa wa Kaskazini Pemba leo wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo uwanja wa Mpira Micheweni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Wingwi Khamis Shaame Hamadi katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo uwanja wa Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Konde Ramadhan Omar Ahmed katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo uwanja wa Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
3
Wananchi na WanaCCM pamoja na Wapenzi wa Chama cha Mapinduzi waliofurika katika Uwanja wa Mpira Micheweni wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akimwaga sera za CCM katika mkutano wa Hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo uwanja wa Mpira Micheweni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni