.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 4 Septemba 2015

JAJI AAGIZA AFISA ALIYEKATAA KUTIA SAINI HATI YA MASHOGA AFUNGWE

Jaji mmoja nchini Marekani amemuagiza afisa wa Kentucky kufungwa jela kwa kukaidi amri ya mahakama baada ya kugoma mara mbili kutoa hati ya ndoa kwa wanandoa mashoga.

Afisa huyo Bi. Kim Davis amesema kuwa kwa imani yake ya Kikristo atakuwa amefanya kosa lisilo na msamaha kwa kukubali kutia saini katika hati ya ndoa ili kuridhia ndoa hiyo ya wanandoa mashoga.

Hata baada ya Jaji kusema kuwa atamuachia huru Bi. Davis ambaye ni karani mkuu iwapo atatoa ruhusa kwa makaimu wake kusaini hati ya ndoa hiyo ya mashoga, bado alikataa kutoa ruhusa hiyo.

Mahakama Kuu ya Marekani iliridhia ndoa za mashoga kukubalika kisheria nchini Marekani tangu mwezi Juni.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni