Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendelea (Chadema) Dk. Willibrod Slaa amevunja ukimya hii leo
kuhusiana na chama hicho kwa kuwashutumu viongozi wa chama hicho kwa
kuwakumbatia wagombea waliokimbilia Chadema kutoka CCM.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari alioufanya leo
Jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa amesema yeye alitangaza hadharani kuwa
Chadema haitopokea tena wagombea makapi, lakini viongozi wenzake
wakaamua kumeza maneno yao na kuamua kuchukua makapi.
Akizungumzia suala la yeye kujiuzulu
wadhifa ndani ya Chadema Dk. Slaa amesema aliandika barua mara mbili
za kujiuzulu ambapo moja wapo alimuandikia Makamu Mwenyekiti wa
Chadema Prof. Abdalah Safari, na kwa sasa yeye hana chama chochote
cha siasa.
Aidha, Dk. Slaa ametumia mkutano huo
kukanusha tuhuma kuwa mkewe Josephine Mushumbushi amepokea fedha ili
amshawishi yeye kukisaliti Chadema na kumkataa Mh. Edward Lowassa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni