.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 2 Septemba 2015

KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA, BAN KI MOON AFUNGUA MKUTANO WA MASPIKA WA MABUNGE DUNIANI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akifungua mkutano wa Nne wa Maspika wa Mabunge Duniani, siku ya Jumatatu, kulia kwake ni Rais wa IPU Bw. Saber Chowdhury na Katibu Mkuu wa IPU Bw. Martin Chungong
Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ann Makinda akiwa na ujumbe wake akifuatilia kwa makini hotuba za ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Maspika wa Mabunge Duniani ulioanza siku ya jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa mataifa
Maspika wa Mabunge kutoka Mataifa yanayoendelea na yaliyoendelea wakiwa katika ufunguzi wa Mkutano wao wa Nne ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano. Ufunguzi wa Mkutano huu umefanyika katika Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

                                                                                Na MwandishiMaalum, New York
 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mewaasa Maspika wa Mabunge Duniani kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa Malengo na Ajenda Mpya za Maendeleo Endelevu, kwa kushirikiana na Serikali zao na Asasi za Kijamii.
 

“ Mnakutana katika kipindi ambacho dunia inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya wimbi kubwa la wakimbizi wanaokimbia vita na machafuko katika nchi zao, wimbi ambalo halijawahi kutokea tangu vita kuu ya pili ya dunia”.

Ban Ki Moon ameyasema hayo siku ya jumatatu wakati akifungua mkutano wa Nne wa Maspika wa Mabunge Duniani ambao hufanyika kila baadaya miaka mitano. Mkutano huu wa siku tatu unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na umeandaliwa na Chama cha Kimataifa cha Wabunge ( IPU).

Na kuongeza. “ Tunachagizwa kuimarisha jitihada na juhudi za kuhubiri Amani, usalama, maendeleo endelevu na haki zabinadamu duniani kote”.



“Watu wanataka elimu, wanataka huduma bora za afya, nafursa zaidi za ajira. Wanataka kuishi pasipo kuwa na hofu. Wanataka kuziamini Serikali zao na Taasisi zake. Wanataka kuheshimiwa kwa haki za binadamu na haki ya kuzungumza nakusikilizwa katika maamuzi yanayohusu maisha yao ”akasema Ban ki Moon.
 

Maspika wanaohudhuria mkutano huu, wanatoka katika mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea. Ujumbe wa Tanzania, unaongozwa na Mhe. Anna Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Na pengine jambo muhimu kwenu na ambalo linawiana na majukumu yenu ni hili. Hiki ni kipindi ambacho mifumo ya kiserikali katika sehemu kubwa ya dunia inakabiliwa na changamoto ya kukosa kuaminiwa, uwakilishi na ushiriki” anaeleza katibu Mkuu

Akizungumzia kuhusu ajenda na malengo mapya ya maendeleo, Ban Ki Moon amesema kuwa malengo hayo ambayo yapo 17 yamelenga zaidi katika maisha ya watu na sayari dunia. Na yanatoa mpango wa utekelezaji katika kumaliza umaskini, njaa na kujenga maisha yenye hadhi kwa wote bila ya kumwacha yeyote nyuma.

Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema lengo namba 16 linazungumzia demokrasia, kwa kutoa wito jamii na taasisi jumuishi. Na kwamba suala la demkorasia limetawala katika andiko lote la malengo mapya ya maendeleo kama upande wa fedha kwa kutia msisitizo wa upatikanaji wa raslimali, huduma za afya, elimu na fursa za ajira na zenye hadhi kwa wote.

Akasisitiza kwamba kazi ya kutekeleza na kusimamia malengo haya ni kubwa, inayohitaji Serikali kufanya kazi na kwa ushirikiano wa karibu na Asasi za Kijamii, uhusiano ambao anasema una toweka ama haupo kutokana na baadhi ya nchi kuweka masharti magumu dhidi ya Asasi za Kijamii.

Mbali ya Ban Ki Moon, viongozi wengine waliozungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huu wa Maspika wa Mabunge ni pamoja na Rais wa Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa.

Baada ya ufunguzi Maspika waliendelea na majadiliano ya jumla yaliyojikita katika maudhui ya Amani, demokrasia na maendeleo endelevu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni