.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 27 Septemba 2015

KONGAMANO LA WANAWAKE WA VYUO VIKUU NA WATAALAM KAULI MBIU “WANAWAKE TUMEWEZA,TUPEWE FURSA”

Mgeni rasmi katika Kongomano la wanawake Mhe. Samia Suluhu akiingia katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kusikiliza mada mbalimbali zilizoandaliwa na wanawake wa vyuo vikuu,wataalamu pamoja na wajasiriamali leo Septemba 26, 2015 jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Menyekiti wa Kamati ya Kongamano Bi.Mary Kighalu na kushoto ni Mjumbe wa kamati kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Prof.Bertha Koba.
Mgeni rasmi katika Kongomano la Wanawake wa Vyuo Vikuu na WataalamWataalam lenye kauli mbiu ya “Wanawake Tumeweza,Tupewe Fursa” Mhe. Samia Suluhu akiingoza meza kutoa heshima ya kumbukumbu ya kifo kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Mhe.Celina Kombani kabla ya kuanza kwa kongamano hilo jijini Dar es Salaam ,ambapo mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo Elimu na Uchumi,Huduma za jamii na Mwanamke na umilikaji wa Rasilimali.
Mjumbe wa kamati kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Prof.Bertha Koba akisoma risala ya kumkaribisha Mgeni Rasmi katika Kongamano la wanawake wa Vyuo Vikuu na Wataalam ambapo mada mbaklimbali zilijadiliwa ikiwemo Elimu na Uchumi,Huduma za jamii na Mwanamke na umilikaji wa Rasilimali.
Mgeni rasmi katika Kongomano la wanawake wa Vyuo Vikuu na Wataalam Mhe. Samia Suluhu akiongea na wanawake walihudhuria kongamano hilo jijini Dar es Salaam.
Wanawake wajasiriamali,wajumbe wa vyuop vikuu na wataalam wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizowakilishwa katika kongamano la wanawake wa Vyuo Vikuu na Wataalam lenya kauli mbiu “Wanawake Tumeweza,Tupewe Fursa” leo jijini dar es Salaam.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni