.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 17 Septemba 2015

KUELEKEA UCHGUZI MKUU BAADAYE MWAKA HUU, BALOZI SEIF ASISITIZA AMANI NCHINI KUDUMISHWA


Picha na – OMR – ZNZ.

Wanamichezo Nchini ambao ndio kundi kubwa katika Jamii wamekumbushwa wajibu wao wa kushiriki vyema katika kuimarisha suala la Amani ili kulifanya Taifa kuendelea kuwa Kisiwa cha Amani Duniani hasa ikizingatiwa kwamba liko katika kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.

Kumbusho hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akizungumza na Wanamichezo tofauti waliounda Kundi la Mazoezi Jimbo la Konde baada ya kushiriki nao matembezi yaliyoambatana na mazoezi na kuishia katika uwanja wa Michezo wa Okapi katika Kijiji cha Misuka Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Balozi Seif Ali Iddi alisema kwa vile uimarishaji wa Suala la Amani unamgusa kila mwana Jamii juhudi za ziada zinastahiki kuchukuiliwa ili kuwawezesha Wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kawaida za kila siku ikiwemo michezo.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zitahakikisha kwamba Amani ya Taifa inadumu na Wananchi wote wanaendelea kuwa washirika wa Amani hiyo.

Alitahadharisha kwamba tabia ya baadhi ya Watu kujaribu kuichezea amani iliyopo kwa kujaribu kuiga mifano ya Mataifa mengine hasa yale ya jirani ni kujenga misingi mibaya ya kusababisha migogoro itakayozua balaa na migogoro isiyokwisha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wananchi wote Nchi kujenga utamaduni wa kushiriki kwenye mazoezi kwa kujiunga na Vikundi tofauti ili kujenga afya zao sambamba na kuimarisha Umoja na Mshikamano miongoni mwao bila ya kujali itikadi na jinsia zao.

Alisema mazoezi pekee yanatosha kuwa tiba kwa kuondoa maradhi madogo madogo na pia yanasaidia kuchangia kwa asilimia kubwa akili Timamu kwa mtu anayeshiriki mazoezi kila siku.

Katika kuunga mkono vikundi hivyo vya mazoezi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliahidi kusaidia seti za Jezi na Mipira kwa Timu za Mpira wa Kandanda na zile za Pete zilizomo kwenye kundi hilo la Mazoezi.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Bihindi Hamad alisema Wizara hiyo wakati wote inaendelea kushirikiana na wanamichezo wote katika kuhakikisha kwamba Sekta ya michezo inaimarika zaidi.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni