Maandalizi ya mchezo kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Nigeria
(Super Eagles) yamekamilika, ambapo leo Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo wa jumamosi kati huku
kiingilio cha chini kabisa kikiwa shilingi elfu saba tu.
Viingilio vya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya
Afrika (AFCON Qaulifier 2017) kundi G itakua ni VIP A Tsh 40,000, VIP B
Tsh 30,000, VIP C Tsh15,000, Rangi ya Machungwa (Orange) Tsh 10,000, na
viti vya rangi ya Bluu na Kijani Tsh 7,000.
Tiketi za mchezo huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa kesho siku ya ijumaa saa 4 kamili asubuhi katika vituo kumi vifuatavyo:
(i) Ofisi za TFF - Karume
(ii) Buguruni – Oilcom
(iii) Mbagala – Dar live
(iv) Ubungo – Oilcom
(v) Makumbusho – Stendi
(vi) Uwanja wa Taifa
(vii) Mwenge – Stendi
(viii) Kivukoni- Feri
(ix) Posta – Luther House
(x) Big Bon – Msimbazi Kariakooo
TFF inawaomba watanzania, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu kununua
tiketi za mchezo huo katika magari yaliyopo kwenye vituo vilivyotajwa
ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na idara nyingine za
kiusalama wameandaa usalama wa kutosha katika kuelekea kwenye mchezo na
kuhakikisha kila mpenzi wa mpira wa miguu anaingia kushuhudia mchezo huo
salama na kuondoka salama.
Mchezo huo utaanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki
utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Rwanda ambao wanatarajiwa kuwasili
leo jioni pamoja na kamisaa wa mchezo huo.
Waamuzi wa mchezo huo ni Louis Hakizimana (mwamuzi wa kati) Honore
Simba (mwamuzi msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi msaidizi),
Abdoul Karim Twagiramukiza (mwamuzi wa akiba) wote kutoka Rwanda na
kamisaaa ni Charles Kasembe kutoka nchini Uganda.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni