Na Dotto Mwaibale
MATUKIO ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na vyombo vya dola hususan jeshi la polisi hapa nchini yameongeza kufikia asilimia 60 imefahamika.
MATUKIO ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na vyombo vya dola hususan jeshi la polisi hapa nchini yameongeza kufikia asilimia 60 imefahamika.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo -Bisimba Dar es Salaam jana katika sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa LHRC Septemba 26, 1995.
“Matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu kwa vyombo vya dola bado yapo juu ingawa uelewa kwa wananchi kuhusu haki za binadamu ni mkubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma wakati tunaanzisha LHRC” alisema Dk. Bisimba.
Alisema baadhi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na jeshi la polisi ni pamoja na kuua raia na kesi zinapofikishwa mahakama zinashindwa kuendelea kwa madai ya kukosekana kwa ushahidi.
Dk. Bisimba alisema matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na wananchi hasa familia ni asilimia 40 ambapo wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi ya kuua watu wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali pamoja na kuvamia vituo vya polisi na kupora silaha.
Alisema katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa LHRC jamii imekuwa na uelewa mkubwa wa matukio ya kifisadi yaliyowahi kutokea kama Sakata la Epa, Richmond, ununuzi wa ndege ya rais, mfuko wa kufufua uchumi na Escrow.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Jaji Mstaafu Osebia Munuo alitoa pongezi kwa LHRC kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na kutetea haki za binadamu.
Munuo alikiomba kituo hicho na mashirika mengine kuendelea kuhamasisha wananchi waliojiandikisha kujitokeza kwenda kupiga kura wakati utakapo wadia na kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu amani ya nchi yetu.
“Naamini sauti ya kituo cheni cha LHRC ni kubwa hivyo baso muitumie vizuri kuhakikisha makundi yote katika jamii yanashiriki vyema katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu bila ya kubaguliwa” alisema Jaji Munuo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni