.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 3 Septemba 2015

MAALIM SEIF AREJESHA FOMU TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI ZANZIBAR ( ZEC )




Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo amerejesha fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
 

Maalim Seif amerejesha fomu hizo majira ya saa nne asubuhi katika ofisi za tume hiyo zilizoko Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar, baada ya kukamilisha masharti yaliyowekwa na Tume hiyo.
 

Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kula kiapo mahakamani pamoja kuambatanisha shilingi milioni mbili, mambo ambayo ametayatekeleza.
Baada ya kukabidhi fomu hizo kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw. Jecha Salim Jecha, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameitaka tume hizo kufanya kazi kwa uhuru na uadilifu.
 

Amesema kufanya hivyo kutapelekea kufanyika kwa uchaguzi wa amani, huru na wa haki, jambo ambalo litailetea sifa kubwa Zanzibar katika jamii ya kimataifa. Katika hafla hiyo, Maalim Seif ameambatana na baadhi ya viongozi wa Chama hicho wakiwemo Mgombea uwakilishi wa Jimbo la Malindi Mhe. Ismail Jussa Ladhu, Mgombea uwakilishi wa Jimbo la Chukwani Mhe. Mansoor Yussuf Himid na Mratibu wa uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Rashid.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni