.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 18 Septemba 2015

MAMA WA MAMA TUNU PINDA AZIKWA RASMI LEO DAR ES SALAAM

1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (kuhosto) ambaye alifiwa na Mama yake , Hajjat Pili Mlolwa Rehani, nyumbani wa marehemu, Tanata Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015. Kuliani Mama Hasina Kawawa. Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu
2
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba Wapili kushoto na Mama Hasina Kawawa waliokwenda kumfariji kufuatia kifo cha Hajjat Pili Mlolwa Rehani,Mama wa Mama Tunu , nyumbani kwa Marehemu, Tabata Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015.
  4
Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal akimfariji mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wakati alipokwenda Tabata magengeni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa marehemu, Hajjat Pili Mlolwa Rehani ambaye ni mama wa Mama Tunu, aliyefariki Septemba 17, 2015. Kulia ni Mama Hasina Kawawa,watatu kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na wanne kulia ni Naibu Waziri wake Pindi Chana.
5
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimfariji mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wakati alipokwenda Tabata magengeni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa marehemu, Hajjat Pili Mlolwa Rehani ambaye ni mama wa Mama Tunu, aliyefariki Septemba 17, 2015. Kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na wanne kulia ni Naibu Waziri wake Pindi Chana.
9
Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika mazishi ya Hajjat Pili Mlolwa Rehani, Mama wa mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda wakiwa nyumbani kwa marehemu Tabta Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015.Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka , Mpigachapa Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.
3
Baadhi ya waomboezaji walioshiriki katika mazishi ya Hajjat Pili Mlolwa Rehani, Mama Mzazi wa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, nyumbani kwa marehemu jijini Dar es salaam, Septemba 17, 2015.
  7
6
Makamu wa Rais Mohammed Bilal akishiki kubeba jeneza lenye mwili wa Hajjat Pili Mlolwa Rehani,mama yake Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda katika sala ilitofanyika nyumbani kwa marehemu, Tabata Magengeni jijini Dar es salam Septemba 17,2015.
8
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa Hajjat Pili Mlolwa Rehani,Mama wa Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda katika mazizi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es slaam Septemba 17, 2015.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni