.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 6 Septemba 2015

MGOMBEA URAIS WA CHADEMA, MH. LOWASSA ALIVYOUTIKISA MJI WA TABORA

Aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja akiuhutubia Umati wa wakazi wa Mji wa Tabora, waliofutirika kwa wingi kwenye Uwanja wa Town School, kulikofantika Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, leo Septemba 5, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia na kunadi sera zake kwa wananchi wa Mji wa Tabora, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika leo Septemba 5, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, akilakiwa kwa shangwe na wananchi wa mji wa Tabora, wakati akipita kuelekea jumwaa kuu, wakati wa Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, leo Septemba 5, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mke wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa, wakati alipowasini kwenye Uwanja wa Town School, kuhudhulia Mkutano wa Kampeni, leo Septemba 5, 2015.
               Umati wa wananchi wa Mji wa Tabora ukiwa kwenye Mkutano huo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, akimwaga cheche zake katika Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, leo Septemba 5, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, akisisitiza jambo katika Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, leo Septemba 5, 2015.
Chopa iliyompakia Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ikipiga misele juu ya uwanja wa Mkutano, leo Septemba 5, 2015, mjini Tabora.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipanda jukwaani kwa kukimbia mara baada ya kutua na Chopa yake, leo Septemba 5, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Mji wa Tabora, leo Septemba 5, 2015.
                                                                                                           Meza Kuu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akiwasalimia wananchi wa Tabora.
                                                                                                “Mabadilikooooooo……”
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakicheza sambamba na wananchi wa Tabora, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Town School, mjini humo leo Septemba 5, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wake, Mh. Freeman Mbowe, wakati wakitoka kwenye Mkutano wa hadhara wa Kampeni, Mjini Tabora leo Septemba 5, 2015.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni