Mkutano ukiendelea
Watumishi na wafanyakazi wa wilaya ya Rombo, wakimsikilza kwa umakini Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla leo amefanya ziara ya kujitambulisha katika wilaya ya Rombo na kuwahakikishia wananchi na Kamati ya Ulinzi na usalama kuwa uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu, huku akivitaka vyama vya Siasa kuendelea na kampeni zao kwa muda huu na wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura tarehe 25 oktoba .
Alisema yeye akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama na mkoa ana wahakikishia amani kabla ambayo ni sasa, siku ya kupiga kura na baada ya uchaguzi kuwa tumejipanga vizuri ili wananchi wapate haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi, alisema mkuu huyo wa mkoa.
Aidha aliongeza kuwa " Nimeziagiza Kamati za Ulinzi na usalama za wilaya zote kujipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu"
Aidha aliwaambia viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa na uchaguzi ufanyike kwa amani kwani wapiga kura wote, viongozi wote wa vyama vya Siasa, viongozi wa serikali ngazi zote na wagombea wa ngazi zote wanasali misikitini na makanisani, hivyo viongozi wa dini ni Muhimu kuhubiri Amani na kuliombea Taifa
Katika hatua nyingine amewataka watendaji wa serikali wa ngazi zote kuacha kufanya kazi kwa mazoea na wachapa kazi na waache urasimu washughulikie matatizo ya wananchi kwa kasi pasipo kuwazungusha mambo ya njoo kesho yaishe
" Nimekuja tushughulike na kero za wananchi na ili mnielewe Hapa ni Kazi tu sitaki uzembe na urasimu hata kidogo".
Amempongeza mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo na Kamati ya Ulinzi na usalama kwa kusimamia vizuri ukomeshaji unywaji wa pombe kiholela na utengenezaji pombe haramu huku akiagiza zoezi hilo liendelee
" Hatuwezi kuwa na Taifa la watu wasiofanya kazi lazima tufanye kazi kwanza na siyo kunywa pombe muda wote" alisistiza.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla akisalimiana na wajumbe Kamati Ulinzi na usalama Rombo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni