Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz, Juliana Ntemo (kushoto) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia) wakati wa ufunguzi wa maonyesho.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akikata keki ya kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni ya kuuza na kununua magari ya Cheki.co.tz. Kushoto ni Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus akiwa na Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz, Juliana Ntemo (katikati).
Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus (kushoto) akimlisha keski mgeni rasmi wa maonesho hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia).
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo(kulia) akimlisha keki Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus baada ya kampuni ya Cheki.co.tz kutimiza mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akimlisha keki Bw. Ally Nchahaga kwa niaba ya watu wote waliofika kwenye ufunguzi huo.
Bw. Ally Nchahaga ambao ni waandaaji wa tamasha la magari Tanzania (Autofest) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika viwanja vya Biafra Jijini Dar. ![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0aN5s8cV4JFxioJknQS1bw7PU8ZKcRYZueVGrViMH19a2GYsJnSaBR83Kr9ZnDAJuXSuh77IdvHmUuKFRqwJwX9t-1SscRn3Yc5bUJrUlFP9pSNVDxpwmrddvyssgwdd6t8iJg23i83kn/s640/DSC_0228.JPG)
Tarehe 19 Mwezi wa septemba 2015 Mtandao wa magari unaoongoza nchini Tanzania Cheki.co.tz
umetimiza mwaka mmoja wa utoaji huduma ya kipekee na iliyo salama ya
biashara ya kuuza na kununua kwa njia ya mtandao pande zote za Tanzania.
Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa utendaji wetu, maelfu ya watu
wamekuwa wakitembelea tovuti yetu kila siku na maelfu ya magari
yamenunuliwa.
Msingi wetu wa wateja umeongezeka mara 21% tangu uzinduzi .
90% ya wafanyabiashara wa magari nchini utumia mtandao cheki.co.tz kuuza magari yao na zaidi ya 50 ya majengo ya kuuzia magari nchini yana nembo ya Cheki.co.tz
katika sehemu zao “Nayaweka mafanikio yetu katika mambo mawili:
Kwanza,
unatokana na urahisi wa kununua, kwani tumewezesha wateja kununua gari
wakati wowote, na mahali popote wanapohitaji. Sababu ya pili, ni
mahusiano mazuri na wauzaji wa magari uliotokana na ubora wa biashara”
alisema Bwana Mori Bencus, Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania.
Naye Juliana Ntemo, Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz
alisema, “ tuna shauku ya kuboresha zaidi huduma yetu kwa miaka ijayo
kwa kuendelea kutoa huduma ya uuzaji na ununuzi kwa njia ya mtandao
iliyo salama na ya kipekee kabisa”.
Ushuhuda wa kipekee kutoka kwa
wateja kwa mwaka 2015 Cheki wameturahisishia biashara, tunapata wateja
kutoka nchi nzima.
Wateja wanaingia moja kwa moja cheki.co.tz na kuona magari yakiwa na maelezo muhimu,na kama mtu anahitaji anawasiliana nasi- Ramadhani Makame, Planet Motors Cheki.co.tz ni
duka la kimtandao, ambapo wanunuzi wa magari na wauzaji wa Kitanzania
hukutana.
Ndani ya tovuti hii magari ya kila aina yanapatikana kwa
wanunuzi Tanzania nzima huku wauzaji wakipata fursa ya kuuza zaidi.
Tembelea www.Cheki.co.tz
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni