Mtendaji Mkuu wa kampuni ya magari
ya BMW, Harald Krueger ameanguka katika mkutano na vyombo vya
hanbari wakati wa maonyesho ya magari ya Frankfurt akiwa amesimama
kando ya gari la BMW aina ya hybrid electric i8 super car.
Muda mfupi tu baada ya kupanda
jukwaani, Krueger alitereza kwa nyuma na kuanguka chini, ambapo
wafanyakazi wawili wa kampuni ya BMW walimkimbilia kumnyanyua ili
kumsaidia kusimama na kuhairishwa kutangazwa kwa gari hilo.
Mtendaji Mkuu wa BMW akiendelea kuanguka
Hapa Bw. Harald Krueger akiwa chali chini
Wafanyakazi wa BMW wakimsaidia kunyanyuka bosi wao




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni