Mwili wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa
Uganda, Jenerali Aronda Nyakairima aliyefariki dunia nje ya nchi
umewasili kwa ndege leo mchana ukitokea Dubai.
Mwili Aronda ambaye aliwahi pia kuwa
Mkuu wa Jeshi la Uganda umewasili majira ya saa saba na nusu mchana
na kupokelewa na mkewe, watoto wake, ndugu wa karibu, viongozi wa
serikali na wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Uganda.
Marehemu Jenerali Aronda Nyakairima
ambaye alikuwa ni mwanajeshi mwenye ujuzi wa hali ya juu, alifariki
dunia jumamosi iliyopita akiwa njiani kurejea Uganda.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni