Mpambano huo wa raundi kumi ulioratibiwa na Kocha wa kimataifa nchini Rajabu Mhamila 'Super D' utakuwa ni wa kumaliza ubishi baada ya mpambano wa kwanza Dimoso kudundwa kwa point.
Super D aliongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mipambano mingine mikali itakayowakutanisha mabondia mbalimbali nchini, ambapo bondia Seleman Zugo atapambana na Abdallah Ruwanje na Adam Ngange atakabiliana na Shabani Mtengela na Said Uwezo atapambana na Hassan Mgosi uku Hamza Mchanjo ataoneshana kazi na Ally Maiyo mipambano yote ya utangulizi ni ya raindi sita.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni