Timu ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles) inatarajiwa kuwasili kesho alhamis saa nne usiku kwenye uwanja wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kwa usafiri wa ndege binafsi tayari kwa mchezo dhidi ya Tanzania siku ya jumamosi uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Nigeria (NFF), kupitia kwa Toyin Ibitoye msafara huo unatarajiwa kuwa na wachezaji 23 pamoja na viongozi wa benchi la ufundi linaloongozwa na kocha mkuu Sunday Oliseh pamoja na viongozi wengine waandamizi wa shirikisho hilo.
Nigeria inatarajiwa kufanya mazoezi siku ya ijumaa saa 10 jioni katika uwanja wa Taifa, ikiwa ni mazoezi mepesi ya kuelekea kwenye mchezo huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni