Hatimaye mtuhumiwa wa mauaji ya
mfanyabiashara wa mabegi soko kuu Jijini Arusha, Alfred Kimbaa (18),
maarufu kwa jina la Mandela aliyekutwa amechinjwa katika hotel ya A.
Square Belmont, huku mwili wake ukiwa hauna baadhi ya viungo kama
kichwa, sehemu za siri, viganja
vya mikono yake na
matiti,amepatikana.
Mtuhumiwa huyo amefahamika kwa jina
la Eligius Edward Lyatuu (31), ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tano,
katika chuo cha Falsafa cha Kanisa Katoliki, kilichopo Segerea Jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Liberatus Sabas,
amesema kuwa mtuhumiwa huo alifanya mauaji hayo, Agosti 30 mwaka huu,
katika chumba cha hotel hiyo na kasha kutoweka na viungo hivyo.
Sabas amesema baada ya uchunguzi
wao kwa kushirikiana na wananchi wenye mapenzi mema na jeshi hilo,
Septemba Mosi, walimkamata mtuhumiwa huyo, eneo la Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) na baadaye alikwenda kuonyesha viungo hivyo,
alikoficha, pembeni mwa mto Mission uliopo Usa river Wilayani
Arumeru.
Amesema chanzo cha mauaji hayo ni
ugomvi kati yao yaani marehemu na mtuhumiwa, ambao hakutaja kwa madai
ni moja ya vielelezo mahakamani.
Kamanda Sabas amesema mtuhumiwa
alifika Arusha akitokea chuoni Dar es Salaam na kuishi nyumbani kwa
marehemu Mianzini na mtuhumiwa ni kaka wa mwenye duka alilokuwa
akiuza marehemu.
Amesema viungo hivyo vimeunganishwa
katika mwili wa marehemu na uchunguzi umefanyika jana, ili ndugu zake
wachukue kwa mazishi na baadaye mtuhumiwa atafikishwa mahakamani
wakati wowote.
Awali mwili wa marehemu huo ulikutwa
katika moja ya vyumba vya hotel maarufu iliopo Jijini hapa, ukiwa
hauna baadhi ya viungo vya mwili kama kichwa, sehemu za siri, viganja
vya mikono na matiti, huku nguo zake alizovaa pia kutoonekana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni