.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 6 Septemba 2015

REGGAE TIME YA PRIDE FM.....JUSTINE KALIKAWE

 
Ni zaidi ya miaka 12 sasa tangu kuondokewa na mwanamuziki mahiri wa Reggae kutoka nchini Tanzania, Justine Kalikawe.

Kwanguni kumbukumbu “mbichi” ya kuondoka kwake, kwa kuwa alifariki tukiwakwenye mkakati wa kufufua hamasa na umuhimu wa muziki wa reggae nchini.

Nakumbukailikuwa ni mwaka 2003. Mwaka ambao ulikuwa na mambo mengi saana kwangu.
 
Ndio mwaka ambao nikiwa na Dj Fax (wakati huo sote tukiwa 100.5 Times
Fm) tulipanga mikakati ya kuwa na kipindi bora zaidi cha Reggae jijini
Dar (ambako radio hiyo ilikuwa ikisikika).

Na nakumbuka tulipangakukutana na kushauriana na wadau mbalimbali wa Reggae nchini kuhusunamna tunavyoweza kushirikiana kuunyanyua muziki huo uliolenga katikaKUELIMISHA, KUBURUDISHA na KUIKOMBOA AKILI YA JAMII ya wanyonywaji. 
 
Nikatika harakati hizo nilipoweza kuonana na kufanya mahojiano na wasanii
kama Jah Kimbute, Ras Inno na nikakosa nafasi kuonana na Justine
Kalikawe ambaye alikuwa akikosekana kutokana na ratiba yake ya kurekodi.
 
Hivyo nikawa “namvizia” ili kujua muda ambao hashiriki kurekodi nimpate
naye aweze kuizungumzia tasnia ya Reggae nchini Tanzania.

Bahatimbaya Justine aliondoka na kwenda nje ya nchi kwa zaiara ya kimuziki naaliporejea hakukaa muda mrefu akakutwa na mauti. Huo ndio ukawa mwishowa ushiriki wake katika mkakati huo.

Lakini wakati anafariki,nilikuwa likizo Bukoba, hivyo siku hiyohiyo nilipata taarifazilizonishtua sana, lakini nikazikubali na kuanza mikakati ya kushiriki
mazishi yake, jambo ambalo nililifanikisha.

Lakini…. Justin Kalikawe ni nani?

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni