.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 6 Septemba 2015

UZINDUZI WA KAVASHA CLUB NA KITABU CHA JIFUNZE LINGALA MTUNZI TCHIMANGA ASSOSSA

Uzinduzi wa Dar Kavasha Club pamoja na uzinduzi wa kitabu cha kujifunza
Kilingala utafanyika leo tarehe 05-Sep-2015 kuanzia saa 12 jioni katika ukumbi wa MRC Mikocheni, ukumbi ulio nyuma ya Shopperz Plaza. 
 
Uzinduzi huo utasindikizwa na burudani kutoka kwa wana Bana Marquis bendi inayoongozwa na mwanamuziki Tshimanga Kalala Assosa, ambaye pamoja na kuwa ni kati ya wanamuziki waliokuweko katika enzi ya uanzishwaji na ukuaji wa mtindo wa Kavasha, akiwa mwanamuziki wa bendi kama Negro Success, Lipualipua, Orchestra kamale, na Orchestra Fuka fuka.
Uzinduzi huu ulikuwa ufanyike mwezi wa 5 lakini ukaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ambapo uzinduzi huo ulipangwa kufanyika.

Kiingilio cha onyesho hili ni BURE. Na hakika tukio hili ni la aina yake katika tasnia ya muziki wa dansi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni