.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 23 Septemba 2015

VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YAFANYA MKUTANO NA WAMILIKI PAMOJA NA WAKUU WA VYUO VYA UFUNDI STADI


                               
                                                                                                    Na Mwandishi wetu

Kongamano la wakuu wa vyuo pamoja na wamiliki wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam lafanyika jijini Dar es Salaam kwa ajiri ya kupeana maelekezo kwa vyuo vilivyo pata usajiri wa awali ili waweze kupata usajiri wa kudumu vilevile kupewa hisibati na namna gani waweze kufuata taratibu ili kupata usajiri huo wa kudumu. 

Mwenyekiti wa bodi ya VETA kanda ya Dar es Salaam Mwalimu Charles Philemon akiongea na wamiliki na wakuu wa vyuo vya ufundistadi kuhusiana na wamiliki hao kupata usajili wa kudumu kwani wao kama VETA familia wanauhitaji wa kutambua na haki ya kupata hisibati inayoonyesha aina ya kozi zinazotolewa na chuo husika kilichopo katika mfumo wa VETA, pia alisema wana mambo muhimu ambayo yanayopaswa kukumbushana ni pamoja na wanayotekeleza, kwani wao nia yao ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi kwa uhakika ili wao waweze kuwa mabalozi wazuri katika kazi zao wawapo nje , tuendelee kujenga mambo ya stadi za kazi katika vyuo vyetu ili kuwahakikishia wananchi kuwa tunaendelea kutoa wakufunzi wenye sifa zinazostahili lakini yote haya yanatokana na kuwa na chuo chenye usajili wa uhakika na wakufuata taratibu za mamlaka ya VETA.

Kwani watu mbalimbali hupimwa kutokana na stadi zao mbalimbali wanazozipata katika vyuo vyetu na kwenda nazo katika kuzitekeleza maeneo tofauti , watu hao ambao wamepita kupitia katika mafunzo ya ufundi stadi VETA ndio watu wenye stadi za kazi kwani hutenda kazi kutokana na elimu mkubwa wanaoupata katika mafunzo yao kupitia vyuo mbalimbali vyenye usajili wa VETA. anasema“kutokana na semina zinazoendelea najua sisi ni familia moja hata kama katika familia kuna watoto warefu na wengine wafupi lakini wote ni watoto wa VETA tufanye kazi kwa umoja ili kutoa vitu vilivyobora zaidi kutofautisha na aina nyingize za utoaji mafunzo, kwani ninaamini walimu wenye ubora ndio wanaopatikana katika mamlaka ya VETA”

Pia aliweza kusisitiza fursa ya kujengana kwa kutembeleana baina ya chuo kimoja na chuo kingine kwa ajiri ya kupata ufanisi zaidi katika mafunzo mbalimbali pamoja na fani kwani familia inajengwa kwa kuwa na uhusiano mzuri na uzuri wa familia huonekana ndani ya VETA ni pale watu mnavyofaidika katika mambo mbalimbali iwe kwa kujengana na kusaidiana kwa kuinua kile kinacho patikana kwani muda mwingi huwa tunakutana mara moja katika maonesho mbalimbali lakini familia hii ya VETA ni mamlaka inayo unganisha vyuo mbalimbali.

Naye mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Bwana Habibu Bukko alisisitiza kuhusiana na kusajiliwa pamoja na kupata Hisibati itakayo saidia katika vyuo vyetu, hivyo aliweza kusema baada ya kupata usajili ndani ya miezi kumi na mbili (12) ni lazima kila chuo kiwe kimepata hisibati kwa wale wote waliokamilisha usajili huo wa mafunzo ya ufundi stadi, pia aliweza kuzungumzia nini maana ya ambapo alisema HISIBATI ni kutambua zile fani ambazo zinatolewa na chuo au umahili wachuo chako upo kwenye fani zipi.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni