Baadhi ya wakazi ya kata wa kisarawe wakifuatilia kwa makini mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo wa ajenda ya watoto ullohusisha wagombea wa udiwani kupiitia vyama vya ccm na chadema
Mmoja wa wananchi wa kata ya kisarawe akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto kuelekea uchaguzi mkuu ambapo ulihusisha wanafunzi na wagombea wa udiwani wa kata hiyo
Mwanafunzi Amina Joka akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo wanafunzi wa shule za Msingi chanzige A ,chanzige B na kisarawe na wagombea wa udiwani kupitia vyama vya ccm na chadema walishiriki
Ndg
Abel Mudo ambaye ni mgombea wa Udiwani kupitia CCM akichangia katika
mdahalo wa ajenda ya watoto kuelekea uchaguzi mkuu ambapo wanafunzi wa
CHANZIGE ,na kisarawe
Ajenda
ya watoto ilianzishwa na mashirika ya watoto Tanzania yakiongozwa na
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa nia ya kuhakikisha
maswala ya watoto na haki zao yanawakilishwa vyema katika serikali ya
Tanzania.
Katika
kuhakikisha kwamba Ajenda za watoto zinazungumzwa katika jamii Kipindi
cha redio cha Walinde Watoto leo kimeandaa mdahalo uliowahusisha
wagombea wa udiwani kata ya Kisarawe ambao ni Abel Mudo (CCM) na Baraka
Musa (CHADEMA) na wakazi wa Kata ya Kisarawe ili kujadili changamoto
mbalimbali zinazowakabili watoto na mipango ya vyama vyao katika kutatua
changamoto hizo.
Mdahalo
huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe
ulihudhuriwa na wenyekiti wa vijiji, na vitongoji, walimu, maafisa
ustawi wa jamii pamoja na wananchi wakazi wa Kata ya Kisarawe.
Akiinadi
Ilani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo, Baraka Musa anayegombea
udiwani kata ya Kisarawe, alisema chama chake kinaamini kuwa lishe bora
ni muhimu kwa ustawi wa watoto kiafya na kielimu na akasema endapo
kitaingia madarakani kitahakikisha kinawekeza kwenye kupata Katiba
inayotambua na kutaja moja kwa moja haki za watoto.
Naye
mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi Abel Mudo alisema endapo chama chake kitapata ridhaa ya
kuendelea kuongoza nchi kitawekeza zaidi katika shule na kuhakikisha
zina walimu wa kutosha na kwamba serikali yake imetengeneza mazingira
rafiki na kutoa zana kwa watoto wenye ulemavu.
Mgombea
huyo aliahidi kwamba watafanya kazi pamoja na wadau mbalimbali ili
kuhakikisha wanapunguza ukatili kwa watoto na kukabiliana na matatizo
ya mimba za utotoni sambamba na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa hadi
kidato cha nne.
Mwanafunzi
Amina Joka aliwataka wagombea udiwani hao pindi mmoja wapo
atakapochaguliwa, wahakikishe wanajenga hosteli za wanafunzi kufikia
kwani kwa sasa wanalazimika kusafiri umbali mrefu sana kwenda shule hali
ambayo ni hatarishi kwani wanakutana na vishawishi vingi njiani.
Katika
hatua nyingine, wagombea hao walipata fursa ya kusikiliza kero za
wanafunzi kutoka shule za msingi Chanzige A, Chanzige B na Kibasila
wilayani kisarawe ambao walitaja kero za upungufu wa walimu, ukosefu wa
huduma za afya, adhabu za mashuleni na ukosefu wa maji kama kero zao za
mda mrefu. “Mgombea bora ni Yule atakayetuletea maji kwani tunaenda
kutafuta maji umbali mrefu badala ya kujisomea” Alisema mwanafunzi
mmoja.
Unaweza
kusikiliza kipindi cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio
shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi
kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org
|
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni