Watafiti wamesema programu kubwa ya
kukabiliana na minyoo kwa binadamu inahitajika ili kuua minyoo hatari
na yenye kukera iliyopo kwenye miili ya watu bilioni 1.5 duniani.
Timu ya Chuo Kikuu cha Stanford
imesema Shirika la Afya Duniani linahitaji kuongeza jitihada zake,
lakini lenyewe limesema kunauwezekano wa kuongezeka usugu wa minyoo
kwa dawa.
Hivi sasa uteketezaji minyoo
umejikita zaidi kwa watoto waliomashuleni katika maeneo
yaliyoathirika mno na minyoo, lakini timu ya Chuo Kikuu cha Stanford
imependekeza zoezi hilo kuhusisha idadi kubwa ya watu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni