.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 16 Oktoba 2015

BENKI YA POSTA YABORESHA ZAIDIN HUDUMA ZAKE, MTEJA ATATOA MAONI BILA KUANDIKA KWENYE KARATASI, NI "KUBOVYA TU" KWENYE MASHINEAKATHE

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi(wapili kulia), akihudumia wateja kwenye tawi la benki hiyo Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa Oktoba 16, 2015, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

                                                                                                     NA K-VIS MEDIA
 
KATIKA kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, Benki ya Posta Tanzania, imeweka mashine maalum ambayo wateja wa benki hiyo wanaofika kupatiwa huduma watatoa maoni yao juu ya huduma wazipatazo kwa kubonyeza vitufe vinavyoelekeza nini maoni yake juu ya huduma aliyoipata.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo, kwenye tawi lake la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Oktoba 16, 2015, Aisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema, benki yake imelenga kutoa huduma zilizo bora na za kisasa ili kurahisisha utendaji wake wa kazi.
 
Moshingi ambaye aliongoza maafisa wa benki hyo kutoka makao makuu kwa kutoa huduma kwa wateja, kuwasikiliza na kuwasaidia namna ya kujaza fomu na kutoa pesa, alisema,hatua ya yeye kuongoza maafisa wake kutoa huduma, ni kuwaonyesha wateja kuwa benki yao inawajali.
 
“Ili kufanikisha lengo hili benki imeanzisha matumizi ya mashine za kisasa zitakazomuwezesha mteja kutoa maoni ya jinsi gani anafurahia au kutofurahia huduma zetu bila kuhitaji kuandika kwenye karatas, mteja atabofya kitufe ili kupata maoni yake, nasi tutayafanyia kazi maoni yake haraka iwezekanavyo.”i.” Alisema Moshingi.
Alisema matumizi ya mashine hizo yataboresha utoaji huduma za kibenki, na hivi sasa mipango ya kuziweka kwenye kila tawi inaendelea.
 Moshingi akimuelekeza mteja namna ya kujaza fomu za kuweka pesa
Afisa wa operesheni wa TPB tawi la Kijitonyama, Agatha Ngoile, (kushoto), akimuhudumia mteja
Frank Mushi (kulia), Meneja wa biashara wa TPB, akiwa na maafisa wengine kwenye eneo la kusikiliza na kupokea wateja kwenye tawi hilo
Mteja akibonyeza kitufe kutoa maoni yake baada ya kupata huduma
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, akibadilishana mawazo na Meneja wa shirika anayeshughulikia mawasiliano, Norvis Moses
Moshingi, (wapili kushoto), akizungumza na Norvis, huku Meneja wa tawi la TPB, Kijitonyama, Emmanuel Kimola akiteta jambo na Afisa Habari Theo Mwakifulefule
Meneja Masoko wa TPB, Deo Kwiyukwa, (kushoto), Meneja Biashara, Frank Mushi, (katikati), na Afisa Masoko, Grace Majige, wakibadilishana mawazo
Moshingi akimkaribisha mteja tayari kumuhudumia
Agatha akiwa kazini
Moshingi akiwa anahudumia mteja kwenye teller

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni