Bunge dogo la Rwanda limepitisha
mabadiliko ya Katiba yatakayo muwezesha rais Paul Kagame kuwania
muhula watatu mwaka 2017, jambo litalomfanya aendelee kukaa
madarakani hadi mwaka 2034.
Akiongea baada ya uamuzi huo spika
wa bunge hilo, Donatille Mukabalisa amewashukuru wabunge wote
walioshiriki katika mchakato huo hadi mwisho, na kusema kazi hiyo
imezingatia matakwa ya watu wa Rwanda.
Mabadiliko hayo ya Katiba yatabidi
yapigiwe kura katika bunge la juu la Rwanda, kabla ya kufanyiwa kura
ya maoni ya kitaifa, hata hivyo yanatarajiwa kupitishwa kutokana na
bunge la juu kuwa na wapinzani wachache.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni