.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 14 Oktoba 2015

DK MAGUFULI ASHIRIKI KUUPOKEA MWILI WA MAREHEMU DK KIGODA DAR


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akizungumza na vyombo vya habari jinsi alivyomfahamu aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara, marehemu Dk Abdallah Kigoda wakati wa mapokezi ya mwili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dcar es Salaam jioni hii, ukitokea India ambako alipatwa na mauti.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, na Mgombea ubunge Jimbo la Handeni kupitia CCM, marahemu Dk Abdallah Kigoda, ukihamishiwa kwenye gari lingine wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana, ukitokea nchini India ambako alipatwa na mauti. Mwili huo ulikwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, kusubiri kuagwa leo katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.


Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro akimfariji dadake na marehemu Dk Kigoda, Dk Aisha Kigoda.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza akimfariji mjane wa marehemu Dk Kigoda, Rasul Kigoda.
Dk Magufuli akimfariji mtoto wa marehemu Dk Kigoda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Dk Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakati wa mapokezi ya mwili wa marehemu Dk Kigoda Uwanja wa Ndege.
Dk Magufuli akisalimiana na wananchi waliofika kuupokea mwili wa marehemu Dk Kigoda

Dk Magufuli (kulia) akiangalia jeneza lenye mwili wa Dk Kigoda ukishushwa wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege, Dar.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni