Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya mwamvuli wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi Ukawa Highness Kiwia, anatarajia kufungua kesia ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimboni humo kwa madai kwamba haukuwa wa huru na haki kutokana na kugubikwa na changamoto mbalimbali.
Kiwia ambae ameshindwa
kutetea jimbo hilo baada kuchukuliwa na Angelina Mabula kutoka Chama cha Mapinduzi CCM, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na Uchaguzi huo.
Alieleza kuwa katika vituo
mbalimbali jimboni humo kulikuwa na makosa mengi ambayo ni pamoja na uwepo wa vituo hewa, idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kupigia kura pamoja na majina ya wapiga kura kukutwa katika majimbo tofauti na yale waliyojiandikishia.
Katika hatua nyingine Kiwia
alikanusha taarifa kuwa alimtuma mwakilishi kwa ajili ya kusaini fomu ya matokeo kwa niaba yake na kwamba siku ya kutangaza matokeo alishindwa kupokea matokeo hayo na hivyo kuzilai.
Kwa upande wake Tungaraza
Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Victoria Chadema, alisema kuwa zoezi la uchaguzi mwaka huu linapaswa kulaaniwa kwa kuwa halikuendeshwa kidemokrasia kutokana na kukiuka taratibu mbalimbali za uchaguzi.
Katika Matokeo ya Kiti cha
Ubunge Jimboni Ilemela, Mgombea wa CCM Angelina Mabula aliibuka mshindi baada ya kupata kura 85,424 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema Highness Kiwia aliepata kura 61,679 ambapo kwa upande wa Madiwani CCM ilishinda Kata 16 huku Kata Tatu zikichukuliwa
na
upinzani.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI
KUSIKILIZA
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni