.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 21 Oktoba 2015

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR, MAFUNZO YATOLEWA KWA WATU WENYE ULEMAVU PEMBA

Ofisa kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar ‘ZEC’ ofisi ya Pemba Suleiman Daud Mkasha ‘kushoto’ akiwasilisha mada katika mafunzo juu ya haki za watu wenye ulemavu kisiwani Pemba kuelekea uchaguzi mkuu, yaliyofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa na kuandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC Pemba, na kulia ni mtoa mada Mohamed Hassan Ali kutoka ZLSC.
Mtoa Mada kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Mohamed Hassan Ali, akiwasilisha mada katika mafunzo juu ya haki za watu wenye ulemavu kisiwani Pemba kuelekea uchaguzi mkuu, yaliyofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa Kusini Pemba, yaliyoandaliwa na Kituo hicho
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasioona Zanzibar ‘ZANAB’ Ruwaida Shaaban Khamis, akitoa maelekezo juu ya matumizi ya kifaa kisaidizi cha kupigia kura kwa watu wasioona, katika mafunzo juu ya haki za watu wenye ulemavu, yaliyofanyika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Kusini Pemba.
Watu wenye ulemavu kisiwani Pemba, wakiwa katika mafunzo juu ya haki zao katika uchaguzi mkuu, katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa Kusini Pemba, yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba.  (Picha na Shemsia Khamis, Pemba). Kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni