Ligi ya mabingwa barani Ulaya imeendelea usiku wa kuamkia leo katika viwanja mbalimbali barani humo, na katika mchezo uliowakutanisha Paris St Germain ( PSG ) waliokuwa nyumbani dhidi ya wageni wao Real Madrid toka Hispania, ulishuhudia mchezo huo ukimalizika kwa timu hizo kutofungana. Katika mchezo huo timu zote zilionyesha soka la uhakika.
MUACHE NI SHABIKI WANGU!! Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akimtuliza askari ( aliyevaa koti la Steward ) kutomtoa kwa nguvu uwanjani shabiki aliyekatiza kwenda kumkumbatia na kutii "kiu " yake.
Wao Manchester City wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani usiku wa kuamkia leo wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wageni wao Sevilla waliosafiri kutoka Hispania.
Mabao kutoka kwa Adil Rami aliyejifunga katika dakika ya 3 ya mchezo huo na bao la ushindi lililwekwa kimiani na Kevin De Bruyne katika dakika ya 90 yalitosha kuwapa pointi tatu muhimu Manchester City.
Bao la Sevilla la kufutia machozi lilifungwa na Yevhen Konoplyanka katika dakika ya 30
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo ya mabingwa Ulaya, Manchester United wakicheza ugenini nchini Urusi walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji wao CSKA Moscow.
Wenyeji ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 15 likifungwa Seydou Doumbia, bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili Manchester United walisawazisha bao hilo kupitia kwa Anthony Martial katika dakika ya 65.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni