.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 16 Oktoba 2015

MAALIM SEIF AKUTANA NA MAASKOFU

Na: Hassan Hamad, OMKR
 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesisitiza nia yake ya kuendelea kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar bila ya kujali itikadi za kisiasa, udini, ukabila au eneo mtu analotoka.
 

Maalim Seif ambaye pia ni mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF ametoa kauli hiyo alipokutana na viongozi wa dini ya kikristo waliopo Zanzibar katika kituo cha utengamano Welezo.
 

Amesema akiwa kiongozi wa nchi, atahakikisha kuwa kila mwananchi anapata haki sawa sawa na mwengine na hakuna atakayebaguliwa au kuonewa kwa misingi yoyote.
 

Katika mazungumzo na viongozi hao ambao pia walipata fursa ya kuuliza masuala mbali mbali kuhusiana na ustawi wao, Maalim Seif amesema atahakikisha kuwa anailinda katika ya Zanzibar ambayo inatoa uhuru wa kuabudu kwa wananchi wote.
 

Amesema msingi mkubwa wa Chama chake ni haki sawa kwa watu wote, na kubainisha kuwa suala la chama hicho kuhusishwa ya udini ni propaganda za kisiasa ambazo hazina ukweli wowote.
 

Nae Askofu Daniel Kwilemba amemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kukubali kukutana na viongozi hao na kuwapa ujumbe ambao amesema umesaidia kutoa mwamko kwa Wakristo wa Zanzibar. 

Askofu Kwilemba ameahidi kuufikisha ujumbe huo kwa waumini wa dini ya kikristo waliopo Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, ili waweze kuelewa ukweli kutokana na mitazamo ya watu mbali mbali kuhusiana na Chama cha CUF na mtazamo wa kiongozi wao juu ya mustakbali wa wakristo waishio Zanzibar.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni