Nyota wa filamu ya Fast &
Furious marehemu Paul Walker ameingia katika orodha ya jarida la
Forbes ya mastaa waliokufa wanaoingiza fedha nyingi.
Walker, aliyekufa kwa ajali ya gari
mwaka 2013, ameingiza dola milioni 10.5, katika mwaka uliopita na
anashika nafasi ya tisa.
Mfalme wa Pop marehemu Michael
Jackson anashika nafasi ya kwanza kwa mwaka watatu mfululizo,
akiingiza dola milioni 115, ikiwa ni pungufu na mapato ya mwaka jana
milioni 140 mwaka 2014.
Marehemu Elvis Presley anashika
nafasi ya tatu kwa mastaa waliokufa lakini bado wanaingiza fedha kwa
kupata dola milioni 55.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni