Mbunge nchini Kenya amewasilisha
hoja binafsi ya kutaka kuvunjwa kwa chombo kinachosimamia mitihani
Kenya, na kuteuliwa wajumbe wapya wa chombo hicho.
Mbunge wa jimbo la Mbooni, Kisoi
Munyao amesema Baraza la Mitihani Kenya (KNEC) limeshindwa majukumu
yake, kutokana na mapungufu ambayo yameongezeka kwa miaka kadhaa.
Mbunge huyo amesema Kenya wamekuwa
wakikerwa na taarifa za udanganyifu wa mitihani, na kuongeza kuwa
wakati sasa umefika kwa kuweka mikakati thabiti ya kusimamia mitihani
isivuje.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni