.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 25 Oktoba 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU

x2
Dkt.Maria Mashingo akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2015.
x3
Prof.Elisante Gabriel akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2015,awali Prof.Gabriel alikuwa Naibu Mkuu wa Wizara hiyo.
x4
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Kikwete akimpongeza Bw.Eliakim Maswi mara baada ya kumaliza kula kiapo Ikulu jijini Dar es salaam,Bw.Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara.
x5
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Gabriel (katikati)akipongezwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Sihaba Nkinga (kulia) ambaye amehamishiwa Wizara ya Wanawake,Jinsia na Watoto pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Assah Mwambene (Kushoto),mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
x6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete(Kulia) akiwa katika picha na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika Bw.Zidikheri Mundeme mara baada ya kuapishwa ikulu jijini Dar es Salaam.
x7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete(kulia) akiwa katika picha na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Hab Mkwizu mara baada ya kuapishwa ikulu jijini Dar es Salaam.
x1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete (watano kulia) pamoja na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (watano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu waliyoteuliwa mara baada ya kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam Oktoba 24,2015.

                                                                     Picha zote na Anitha Jonas – MAELEZO.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni