.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Oktoba 2015

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA JENGO LA MAKAZI NA BIASHARA NHC MOROCCO SQUARE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaeka jiwe la msingi la mradi mkubwa wa jengo la makazi na biashara la Morocco Square ambao ni mkubwa kwa eneo hili la Afrika Mashariki ambao umejengwa katika msingi mmoja. Wanaoshuhudia nia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB PLC LTD, Dk Charles Kimei.

Mradi huu una uwezo wa kubeba watu 6000 na kutoa ajira ya zipatazo 24,750. Mradi huu una majengo manne tofauti, ikiwemo ya ghorofa 22 kwa ajili ya nyumba 100 za makazi za vyumba vitatu na vinne, ghorofa 20 na 17 kwa ajili ya Ofisi na maduka makubwa na ghorofa 13 kwa ajili ya Hoteli yenye vyumba vya kulala 81. Mradi huu una eneo maalum la kutua helkopta na eneo kubwa kwa ajili ya maegesho ya magari.
         Jengo la NHC Morocco Square litakavyokuwa mara baada ya kukamilika.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya mradi wa Morocco Square kutoka kwa Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC, Issack Peter
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya mradi wa Morocco Square kutoka kwa Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC, Issack Peter.


Baadhi ya wafanyakazi wa NHC na wageni waalikwa waliokuwapo katika shughuli hiyo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa NHC na wageni waalikwa waliokuwapo katika shughuli hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii Susan Omari akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Zakhia Meghji wakati akiingia katika eneo la tukio.
  Rais Kikwete akiwasili katika eneo lililowekwa jiwe la msingi la Morocco Square.
Rais Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa NHC wakati akiwasili eneo la tukio.
  Rais Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa NHC wakati akiwasili eneo la tukio.
  Rais Kikwete akifuatiliahotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC hayupo pichani wakati akiwasili eneo la tukio.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akisoma hotuba yake kwa Rais Kikwete.
 Msondo Ngoma Music Band walikuwapo eneo la tukio wakitoa burudani
 Rais Kikwete akihotubia kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa NHC Morocco Square.
Wakuu wa Taasisi mbalimbali ambao walialikwa katika shughuli hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi
            Rais Kikwete na Baadhi ya Watendaji wakuu wa Menejimenti ya NHC.
                                                                               akiondoka eneo la Mradi
Baadhi ya wafanyakazi wa NHC na wageni waalikwa waliokuwapo katika shughuli hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni