Moja ya eneo lililoaribika kutokana na hali ya mabadiliko ya tabianchi (Climate Change) katika fukwe ya Kilindoni, katika Kisiwa cha Mafia, Mkoani Pwani, nchini Tanzania. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Afisa Mazingira wa Wilaya ya Mafia, Bw. Gideon Zakayo.
Moja ya vyombo vya uvuvi na usafirishaji abiria vikiwa vimepaki katika fukwe za Kisiwa cha Chole huku vikisubiria maji kurejea katika eneo hilo kama vilivyokutwa na mwandishi wa makala haya. (Andrew Chale).
Pichani ni katika eneo la Fukwe za Wavuvi kama linavyoonekana lilivyoharibika kulikosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo la Kilindoni wameeleza kuwa, miaka ya nyuma hapo palikuwa na minazi huku maji ya bahari yakiwa mbali, lakini kwa kadri mabadiliko yalivyotokea, eneo hilo limeweza kuliwa na kufanya minazi kupotea hali iliyosababisha kuweka mfereji/mto mdogo ambao unapitisha maji kutoka baharini na kuchanganyika na yale ya mvua ya kwenye makazi ya watu. (Picha na Andrew Chale)
Taswira ya kisiwa cha Chole kinavyoonekana..
Baadhi ya fukwe za kupendeza za kisiwani Mafia zinavyookena kwa picha hii iliyopigwa juu
Moja ya sehemu za eneo la Kisiwa cha Jibondo kama inavyoonekana pichani ambapo kisiwa hicho kipo juu ya mwamba ama jiwe kama inavyofahamika Jibondo ama jiwe kubwa. (Picha ya kwa hisani ya Mafia Island page ya fb).
Pichani Mwandishi wa Makala haya akiwa katika boto maalum kwa safari za visiwa vilivyo ndani ya Mafia ambavyo Kisiwa hicho kinakadiliwa kuwa na Visiwa vidogovidogo zaidi ya vitano. Picha ya chini Mwandishi akiwa katika Kibao cha Shule ya Kijiji cha Chole katika Kisiwa cha Chole ambacho ni kisiwa pekee chenye magofu ya Kale na vitu vya thamani vya enzi za zamani vikiwa vimehifadhiwa huko.
Kisiwa cha Chole
Moja ya visiwa vidogo na vya kuvutia ndani ya Kisiwa cha Mafia.Na
Andrew Chale, Modewjiblog
[MAFIA-ISLAND] Kisiwa cha Mafia kijografia kipo karibu na mlango wa Mto Rufiji kusini mwa Tanzania.
Hata
hivyo, Kisiwa hichi ambacho ni Wilaya moja wapo ya Mkoa wa Pwani
inakabiriwa kwa kiwango kikubwa na changamoto za Mabadiliko ya tabianchi
hasa baada ya wananchi wake wengi kutopata elimu hiyo sahihi.
Imeelezwa
kuwa, elimu juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika
Kisiwa cha Mafia ambacho pia kinaunda visiwa vidogovidogo zaidi ya
vitano, wananchi walio wengi katika kisiwa hicho bado hawajapata elimu
sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya kimazingira (Climate Change).
Mtandao
huu ambao ulipiga hodi katika kisiwa hicho cha Mafia ili kupata habari
za mabadiliko ya tabianchi na namna ya Mabadiliko ya tabianchi yanavyo
athiri Kisiwa hicho (How Climate Change effects Mafia Island in
Tanzania) ambapo iliweza kuzungumza na maafisa Ardhi, Mazingira na
wananchi wa Wilaya hiyo, na kueleza haya:
Kwa upande wa Afisa
Mazingira wa Wilaya hiyo, Gideon Zakayo (pichani juu) amebainisha kuwa,
Kisiwa cha Mafia kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za Kimazingira
ikiwemo hali ya Mabadiliko ya tabianchi huku suala la elimu kwa wananchi
likiwa dogo kutokana na kutokuwa na fungu la kutosha.
“Kwa sasa
bado hatuna fungu la kutosha kuwafikia wananchi na kutoa elimu ya
Mabadiliko ya tabianchi. Ila bado milango ipo wazi kwa mashirika na
taasisi binafsi kufika na kutoa elimu hiyo kwa sasa” anasema Zakayo.
Zakayo
ameongeza kuwa, Suala la Mazingira ni pana kwani limejumuisha Afya,
Maji, Kilimo, Misitu, ardhi na mazingira yote kwa ujumla hivyo wadau
wanahitajika kujitokeza kusaidiana na Serikali katika kutoa elimu,
kuelimisha sera na taratibu zinazotakiwa kufuatwa na wananchi katika
maeneo husika.
Aidha, ameongeza kuwa, katika miongoni mwa visiwa
vidogo vidogo ndani ya Mafia, kuna baadhi ya visiwa vimeanza kuharibiwa
kutokana na Mabadiliko ya tabianchi.
“Vipo visiwa baadhi tayari
vimeanza kuathirika na mabadiliko hayo kwani maji yamekula ardhi. Pia
baadhi ya maeneo maji yameweza kuingia katika ardhi na kubadilisha
maeneo hayo tofauti na awali.” amebainisha Zakayo, Afisa Ardhi Wilaya ya
Mafia.
Mahojiano na wananchi kisiwa cha Jibondo:
Modewjiblog
imeweza kufanya mahojiano kadhaa na wananchi wa kisiwa cha Jibondo
ambapo wameweza kueleza kuwa kisiwa hicho kimeanza kulika katika baadhi
ya maeneo kwani kwa sasa maji yameweza kuingia katika ardhi.
Kwa
mujibu wa wakazi wa Jibondo ambapo maana ya jina hilo ni jiwe kubwa na
ndivyo kilivyo kisiwa hicho, kwani kipo juu ya mwamba mkubwa kwa sasa
baadhi ya maeneo maji ya bahari yameingia baharini.
Zahoro Swed
mkazi wa Jibondo amemweleza mwandishi wa habari hizi kuwa, awali katika
eneo wanaposhushia vyombo vya usafiri lilikuwa mbali na majini, lakini
sasa eneo hilo limemezwa na maji yamesogea zaidi.
“Wasiwasi wetu
ni ujaaji wa maji. Zamani vyombo vyetu tulikuwa tunapaki eneo la nyuma
kabisa, lakini sasa tunasogea hadi huku mbele haya ni mabadiliko na hali
ikizidi hivi basi tutakuja kushuhudia maji yakiingia katika makazi ya
watu” alibainisha Swed alipozungumza na Modewjiblog katika kisiwa hicho cha Jibondo.
Aidha,
kwa upande wao baadhi ya wananchi wa eneo hilo la jibondo wamebainisha
kuwa, kutokana na suala la uvuvi kushamiri wapo wavuvi wasio waaminifu
wanaotumia mabomu kiasi cha kuharibu mazingira ya bahari hata kupelekea
kisiwa hicho kupata matatizo ya maji kuingia kwenye ardhi.
Wakazi
hao wameeleza kuwa, elimu ndogo ndio chanzo cha wavuvi hao kuendelea
kutumia mabomu kufanya shughuli zao za uvuvi haramu ambapo mabomu hayo
yanapelekea kisiwa hicho ambacho ni cha miamba ama jiwe (Mafiwe)
kuathirika zaidi huku Mabadiliko ya tabianchi yakipata nafasi ya
kuongeza uharibifu huo.
Kisiwa cha Chole:
Kwa upande wa
wananchi wa kisiwa cha Chole ambacho ni kisiwa kidogo na ndio kisiwa
chenye utalii na urithi wa kale ikiwemo magofu na majumba ya zamani,
wananchi wengi wa kisiwa hicho wamelalamikia juu ya elimu ndogo ya
Mazingira kutolewa licha ya kuihitaji mara kwa mara.
Wakazi hao
wa kisiwa hicho walipaza sauti kwa kueleza kuwa, wengi wao
wanajishughulisha na shughuli za baharini ikiwemo uvuvi na suala la
kilimo cha mwani ambapo wamekuwa wakishuhudia matatizo ya kimazingira
yanayotokea baharini mara kwa mara.
Swaumu Mohammed ambaye ni
mkazi wa kisiwa hicho cha Chole anayefanya shughuli za kilimo cha zao la
mwani anaeleza kuwa wamekuwa wakishuhudia mabadiliko kadhaa ndani ya
bahari hiyo ikiwemo baadhi ya maeneo kuwa tofauti na awali.
“Maji
yamekuwa yakiongezeka mara mbili zaidi. Wakati mwingine tunapofika
kuvua mwani hapa kipindi cha nyuma maji yalikuwa ni ya kiasi, lakini
kuna wakati hali hiyo inakuwa haipo kabisa na maji yanakuwa ni mengi
zaidi na hata kutupa hofu.
Hivyo elimu zaidi inahitajika katika
kujua mabadiliko ya tabianchi ni yapi na namna ya kujikinga nayo hasa
sisi tunaoshinda baharini muda mrefu” alieleza Bi. Swaumu alipoulizwa
kama anafahamu juu ya hali ya mabadiliko ya tabianchi ama .
Mbali
na wananchi wa visiwa hivyo, kwa upande wa wananchi wa Kisiwa cha
Bwejuu kwa upande wao wameonyesha wasiwasi wao kuwa baadhi ya maeneo
yanayozunguka kisiwa hicho yamekuwa yakiliwa na maji kwa muda mrefu huku
kukiwa hakuna juhudi za haraka kunusuru hali hiyo.
Wananchi hao
wameonyeshwa kusikitishwa na kasi ya hali hiyo kwani imekuwa ikiongezeka
mara kwa mara na hakuna hatua ya haraka iliyochukuliwa.
“Kwa
kawaida ukiwa unatoka sehemu moja ama nyingine hali hii hutoiona kwa
harakaharaka. Ila kwa sie tuliozoea ndio tunajua kama ardhi imeliwa na
bahari” anaeleza mmoja wa wavuvi anayefanya shughuli zake katika eneo la
kisiwa hicho aliyefahamika kwa jina la Salum Mwinyikame.
Aidha,
Mwinyikame ameongeza kuwa, kisiwa hicho ambacho ni asili ya mchanga.
Kimekuwa kikipata changomoto nyingi ya kimazingira huku akiomba mamlaka
husika kufika na kutoa elimu hiyo ya mazingira.
Hata hivyo, Modewjiblog
ilipowasiliana na viongozi wa Serikali wa Kisiwa hicho cha Mafia,
wamebainisha kuwa, karibu visiwa vyote vinavyokaliwa na watu wamekuwa
wakijitahidi kufikisha elimu mbalimbali huku akisisitiza wito wa wadau
binafsi kujitokeza kusaidia na serikali katika swala hilo la utoaji wa
elimu ya Mazingira na mabadiliko ya tabianchi hasa katika kukabiliana na
majanga yatokanayo na masuala hayo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni