Nchi ya China imetangaza kuachana na
sera yake iliyodumu kwa muongo mmoja ya wananchi wake kuzaa mtoto
mmoja tu.
Wanandoa wa nchi hiyo sasa
wataruhusiwa kuzaa watoto wawili, imeeleza taarifa ya chama cha
Kikomonisti cha nchi hiyo.
Sera hiyo yenye utata ya kuzaa mtoto
mmoja ilitambulishwa rasmi katika taifa hilo la China mwaka 1979, ili
kupunguza idadi ya watu nchini humo.
Inasemekana sera hiyo imesaidia
kudhibiti kuzaliwa watoto milioni 400, hata hivyo hali ya taifa hilo
kuwa na watu wengi wenye umri mkubwa kwa sasa, imepelekea kufanyika
kwa mabadiliko yake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni