Mjumbe wa TAMWA Zanzibar Bi Shifaa Said akitowa maelezo kuhusiana na mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar kabla ya kuaza kwa mkutano huo uliowashirikisha Wahariri wa Vyombo vya Habari vya Serikali na vya Binafsi Zanzibar.waliohudhuria mkutano huo wa mafunzo ya Uhariri kwa Ajili ya Kuimarisha Amani ya Nchi Inayohusiana na Kuripoti Habari za Uchaguzi Mkuu Zanzibar
Mkuu wa Mradi wa Kusaidia Uchaguzi Salama wa (ECES) Unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya Bi Victoria Florinder, akitowa shukrani kwa Wahariri wa Habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Mnazi Mmoja Zanzibar.
Mkufunzi kutoka Associated Press Ndg Ali Sultan akitoa Mada inayohusiana na Uhariri wa Habari za Uchaguzi kwa Wahariri wa Habari Zanzibar kutoa Habari mbalimbali za Uhakikakatika Vyombo vyao hasa wakati huu wa Uchaguzi Mkuu bila ya kupendelea Upande wowote katika kuripoti habari hizo.
Muandishi Muandamizi Ndg Salim Said Salim, akichangia wakati wa mkutano huo wa Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar.kulia Mhariri Mkuu wa Gazeti la Serikali la Zanzibar Leo Bi Nasma Chum na kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg Chande Omar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg Chande Omar alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo akifafanua jambo wakati wa mkutano huo ukiendelea kwa michango ya Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Mnazi Mmoja Zanzibar.
Afisa wa TAMWA Zanzibar Mzuri Issa akitowa tathimini ya Michango mbalimbali kutoka kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar walioshiriki mkutano huo wa kuripoti habari za Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kuhusu kushiriki kwa Vyombo vya habari kuandika habari za Uchaguzi katika Vyombo vyao, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Mnazi Mmoja Zanzibar.

Mhariri wa Habari wa Gazeti la Serikali Zanzibar Leo Ndg Ramadhani Makame akichangia katika mkutano huo wa Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Mnazi Mmoja Zanzibar.
Washiriki wa mkutano wa kuripoti habari za Uchaguzi Mkuu Zanzibar uliowashirikisha Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar wakifuatilia mkutano huo ulioandaliwa na TAMWA kwa kushirikiana na Shirika la European Center for Electoral Support (ECSE), wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwakilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hya Habari Mnazi Mmoja Zanzibar.
Washiriki wa semina ya siku moja ya Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar kuripoti habari za Uchaguzi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mumalizika kwa semina hiyo iliofanyanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Mnazi Mmoja Zanzibar na kuwashirikisha Wahariri wa Vyombo vya Serikali na Binafsi vya Habari Zanzibar iliofadhiliwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la European Center for Electoral Support kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA. (Picha na Abdalla Omar Maelezo Zanzibar)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni