.
.
.
.
.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga
|
TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.
mbani
NYUMBANI
HABARI
SIASA
MICHEZO
BURUDANI
TABASAMU
KIMATAIFA
Alhamisi, 22 Oktoba 2015
WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA UMOJA WA AFRIKA (AU) WATUA OFISINI KWA WAZIRI CHIKAWE, WAJADILIANA KUHUSU UCHAGUZI MKUU.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando Emilio Guebuza. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (Katikati kulia) akimfafanulia jambo Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando Emilio Guebuza (wapili kushoto), pamoja na wajumbe wenzake, jinsi Tanzania ilivyojipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu utakavyokuwa wa amani. Wakwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), ambaye pia ni Rais wa Zamani wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) wakati Mkuu huyo pamoja na wajumbe wenzake walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, hata hivyo, Chikawe aliwahakikishia kuwa Uchaguzi huo utakuwa wa amani. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni ( Atom )
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni