.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 22 Oktoba 2015

WAFANYAKAZI WA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR WAWAFANYIA TAFRIJA YA KUWAAGA WAZIRI NA NAIBU WAKE

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) waliofika katika sherehe za kuagwa kwao zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. Kushoto Waziri wa AfyaZanzibar Mhe. Rashid Seif Suleiman.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Rashid Seif Suleiman akitoa nasaha zake na kuwashkuru watendaji wake kwa mashirikiano yao katika sherehe za kuagwa kwao zilizofanyika Wizara ya Afya, (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Jidawi na (kulia) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo.
Baadhi ya Mafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakisikiliza nasaha kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) katika sherehe za kuaaga zilizofanyika Wizara ya Afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Rashid Seif Suleiman katika sherehe za kuagwa kwao zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya Zanzibar wakiitikia dua baada ya kumaliza hafla ya kuwaaga Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni