Wahamiaji 22 wengi wao wakiwa ni
watoto wamekufa maji wakijaribu kukatiza kufika Kalymnos na Rhodes
wakitokea Uturuki, hii ikiwa ajali ya pili kubwa ya boti karibu na
visiwa vya Ugiriki, katika wiki hii.
Maafisa wa Ugiriki wamesema watu 19
wamekufa na 138 wameokolewa karibu na Kalymnos.
Watu wengine watatu wamekufa karibu
na Rhodes na wengine watatu hawajulikani walipo, sita wakiokolewa.
Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis
Tsipras amesema anajisikia aibu kutokana na Ulaya kushindwa
kukabiliana vyema na tatizo la wahamiaji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni