.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 3 Oktoba 2015

WANANCHI WAFURAHIA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, AMOS MAKALLA

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla akiongea na waandishi wa habari ( Picha kutoka maktaba )

Na mwandishi wetu, Kilimanjaro.


Wananchi kutoka sehemu mbalimbali mkoani Kilimanjaro wamefurahia kuteuliwa kwa aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla kuwa mkuu wa mkoa huo. 

Wakiongea kwa nyakati tofauti, wananchi hao kutoka maeneo ya Pasua na Majengo wamesema kama mkuu huyo wa mkoa akipewa ushirikiano mzuri na viongozi wenzake ni dhahiri mkoa wa Kilimanjaro utapiga hatua kubwa kimaendeleo. 

Mmoja wa wananchi hao, Aidan Mmari amesema amekuwa akimfuatilia Mh Makalla toka alipokuwa Wizara ya Maji na kuona utendaji wake wa kasi tena kwa vitendo, hivyo ana imani kasi hiyo hiyo amekuja nayo mkoani Kilimanjaro. 

Amemuomba mkuu huyo wa mkoa kufuatilia miradi yote ambayo kasi yake imekuwa ya kusuasua ili Kilimanjaro iendelee kusonga mbele kimaendeleo. 

Mh Makalla ahivi karibuni aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. 

Tayari ameshaanza majukumu yake mkoani humo, na hivi karibuni alifanya ziara sehemu mbalimbali za mkoa huu ikiwa ni pamoja na wilaya ya Rombo. 

Jana Mh Makalla alitembelea wilaya ya Hai na baadaye alielekea Usangi ambako huko pia alikutana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Cleopa Msuya, ambako Waziri Mkuu huo Mstaafu alimpongeza Mh Makalla kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro, na kumtaka kushughulikia kikamilifu matatizo yanayowakbili wananchi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni