.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 22 Oktoba 2015

WANANCHI WAMESEMA COSATO CHUMI KUIJENGA MAFINGA MPYA AKIPEWA RIDHAA

Mgombea ubunge wa jimbo la Mafinga kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Cosato Chumi akiwahutubia wananchi wa ihimbo
                                  Chalamila kampeni meneja akihutubia wanachi wa ihimbo
Mgombea ubunge wa jimbo la Mafinga kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Cosato Chumi akiongea na mlemavu wa viungo kwenye mkutano wa ihimbo.

Na Fredy Mgunda,Mafinga 
 
Wananchi wa kata ya rungemba katika jimbo la Mafinga
mjini wampongeza mgombea ubunge wa jimbo hili kupitia tiketi ya chama cha
mapinduzi (CCM) Cosato Chumi kwa kufanya kampeni za kistaarabu na kuwapa matumaini kuwa atakuwa kiongozi mzuri na kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo.
 
“Tumeona wagombea wengi wakija hapa kupiga kampeni na
kuomba kura kwa njia ya matusi na kuhamasisha kutomchagua kiongozi furani pasipo kutaja au kuongelea hata hoja za msingi kwanini wanaomba kura zetu”walisema wananchi hao
 
Waliongeza kwa kusema kuwa imefika wakati wananchi wanapaswa kuwakata wapinzani katika jimbo hilo kutokana tabia yao kuwafundisha
tabia mbaya wafuasi wao hasa wanapoamua kuanza kuchana mabango ya wagombea wa chama cha mapinduzi (CCM)
 
“Tuliwakamata baadhi ya vijana wakiwa wananchana mabango ya wagombea wa ccm katika kata hii lakini tulipowafikisha kituo cha polisi walisema wanatumwa na viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo
chadema” walisema wananchi hao
 
Wananchi hao wamewasisitia wananchi wa jimbo hilo kutunza
na kuhifadhi sehemu nzuri vitambulisho vyao vya kupigia kura kutokana na tabia inayoanza hivi sasa wanataka namba za vitambulisho na wengine wananunua vitambulisho hivyo wananchi tutajinyia haki yetu ya msingi ya kumchagua kiongozi tunayemtaka kwa kuza vitambulisho vyetu.
 
“Kwa sasa wanapita usiku waki wakitaka kununua vitambulisho vyenu au tuwatajie namba za vitambulisho vyenu na kuahidi kutupa kiasi kikubwa cha pesa ili kufanikisha lengo lao,hivyo tunawaomba jeshi la polisi na mamlaka husika kulizibiti tatizo hilo kabla ya uchaguzi ili wananchi watumie haki yao ya msingi”.walisema wananchi hao
 
Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha mapindizi (CCM) COSATO CHUMI amesema wananchi wanapashwa kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na wapinzani wake kwa kuwalaghai wananchi kwa kununua vitambulisho au kunakili namba za vitambulisho hivyo
.
“Tuwakatae viongozi wa namna hiyo kwa kuwa lengo lao ni kutaka kuununua uongozi kwa nguvu ya pesa na kuwa wao sio chaguo la wanachi hivyo wananchi msidhubutu kufanya hivyo mtapoze haki yenu ya msingi na hampata
kiongozi atakaye waletea maendeleo”.alisema chumi
 
Lakini chumi alisikika akiwaambia wananchi wa kata hiyo tuwakatae wagombea hao wanaohamasisha kuturushia mawe kwenye mikutano yenu
lakini kupiga mawe gari zenu na kuhamasisha vurugu kwa wananchi katika kipindi hiki cha kampeni je mkiwapa madaraka si ndio watawaongoza kwa kutumia mabavu kwa kuwa hata kuingia madarakani wametumia nguvu.
 
“Nawaombeni wanachi wa kata ya rungemba kukipigia kura
cha chama cha mapinduzi (CCM) kuanzia ngazi ya udiwani,ubunge hadi urais kwa kuwa viongozi hao wote wanasifa ya kuwa viongozi wa nchi hii”alisema chumi.
 
Naye kampeni meneja wa mgombea huyo amewataka wananchi kuwataa kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu kutokana na wazazi wao kujilimbikizia mali kipindi baba yake akiwa mbunge kwa takribani miaka
thelathini na sasa wanatumia mali hizo kuwadanganya wananchi na kuwaraghai kwa vijipesa vyao lakini wao hawana aiba ya
kuwa viongozi.
 
Alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua cosato chumi kwa kuwa ni kiongozi mzuri na atawaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni